..FOUNDATION NEWS

Mke wa Rais na Mwenyekiti wa WAMA, Mhe. Mama Salma Kikwete assistiza umuhimu wa elimu katika kupambana na umaskini, Desemba 3, 2010, Dar es Salaam

Mke wa Rais, Mama Salma Kikwete, amesema elimu ni nyenzo muhimu katika kupambana na umasikini, pia amepongeza ongezeko la taasisi za elimu nchini.

Alisema hayo jana (Desemba 3, 2010) jijini Dar es Salaam, alipokuwa akizindua mafunzo ya uuguzi katika Taasisi ya A3 ambayo ni taasisi dada ya shule za Al Muntazir.


Mama Salma, alisema miongoni mwa mambo yanayotofautisha nchi zilizoendelea na zinachoendelea ni kiwango cha elimu.

“Hii ni kwa sababu utajiri na mali havijileti vyenyewe kwa mtu, ni matokeo ya mambo mengine ikiwemo elimu. Kiwango cha elimu na ujuzi ndicho kinachotofautisha nchi zilizoendelea na zile zinazoendelea,” alisema.

Alifafanua kwamba, kwa kadri kiwango cha elimu, ujuzi na maarifa kinavyokuwa juu, ndivyo maisha ya watu katika nchi husika yanavyokuwa bora.

Kutokana na sababu hiyo, alisema, serikali imeamua kuwekeza katika elimu, na katika hotuba ya kuzindua Bunge hivi karibuni, Rais Jakaya Kikwete alisisitiza kipaumbele ni elimu.

Mama Salma alisema, ujenzi wa shule za sekondari katika kila kata, na Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) ambacho kimeshaanza kutoa wahitimu, ni uthibitisho wa dhamira ya dhati ya serikali katika kuinua elimu nchini.

Site Search