FOMU ZA MAOMBI ZA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA SHULE ZA SEKONDARI ZA WAMA SHARAF NA WAMANAKAYAMA
Event Location:
Mitwero Manispaa ya Lindi /Nyamisati Halimashauri ya mji wa Rufiji
Event Date:
17 November, 2016

Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) inatangaza nafasi za kidato cha kwanza kwa wasichana katika Shule zake mbili za sekondari.

(i)Sekondari ya WAMA- Sharaf iliyopo Mitwero katika  Manispaa ya Lindi na

(ii)Shule ya sekondari Wananakayama  iliyopo Nyamisati, Halimashauri ya Mji wa Rufiji

WAMA ni Taasisi isiyo ya kiserikali iliyoanzishwa na Mhe. Mama Salma Kikwete ili kusaidia maendeleo ya wanawake na watoto. WAMA inaendesha shule hizi maalum kwa ajili ya watoto yatima na wanaotoka katika mazingira magumu. Hata hivyo, WAMA inatoa fursa chache kwa wanafunzi wengine ambao wazazi wao wana uwezo wa kulipia ili kuongeza uwezo wa kusaidia watoto wengi zaidi.

Tunafurahi kutoa fursa hii kwa wasichana ambao wataweza kulipia ada kwa kidato cha kwanza katika shule zote mbili kwa mwaka 2017.

Fomu za kujiunga  zimeambatanishwa hapo chini au unaweza  kuzipata  katika ofisi za Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) Dar es Salaam zilizopo Kawe karibu na Hoteli ya Picolo Beach

Kwa wakazi wa Lindi fomu zinapatikana katika Ofisi za Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) tawi la Lindi zilizopo  katika makutano ya Barabara ya Karume na Amani , Kiwanja no.11 kitalu B karibu na  Ofisi za Magereza  za Mkoa wa Lindi

Kwa wakazi wa Pwani Fomu zinapatikana shuleni WAMA Nakayama iliyoko Nyamisati Halimashauri ya mji wa Rufiji

Mitihani ya kujiunga na shule zitafanyika katika shule za sekondari ya WAMA SHARAF  na WAMANAKAYAMA Tarehe 17/11/2016.

Fomu zote pamoja na risiti za malipo ya fomu zirudishwe katika ofisi ya Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) Dar es Salaam zilizopo Kawe karibu na Hoteli ya Picolo Beach.

Kwa wakazi wa Lindi fomu zirudishwe shuleni WAMA Sharaf iliyoko Mitwero Lindi Mjini. Na kwa wakazi wa Pwani Fomu zirudishwe shuleni WAMA Nakayama iliyoko Nyamisati.

Fomu ioneshe shule unayotaka kujiunga nayo (WAMA NAKAYAMA au WAMA SHARAF)

Nakala ya fomu na risiti ya malipo iliyo skaniwa inaweza tumwa kwenda kwenye barua pepe ya Taasisi ya  WAMA ambayo ni: info@wamafoundation.or.tz.mbugunimwajuma@gmail.com na alimindria66@yahoo.com

Mwisho wa nkurudisha fomu ni Alhamisi tarehe 10/11/2016.

Ada au gharama za fomu ni shilingi Elfu ishirini (20,000/=) ambazo hazitarudishwa zilipwe kwenye Akaunti ya  CRDB Namba 0150043016403, Jina la akaunti : WAMA NAKAYAMA

 

Kwa Mawasiliano zaidi:

Piga Namba:  0685-651449, 0789-000341, 0754-439183,

 

 

Terms of Use | Privacy Policy | SitemapCopyright © 2010 - 2018 WAMA Foundation, All Rights Reserved