..FOUNDATION NEWS

Mama Salma aeleza computer itakavyomuinua Mwanamke - March 13, 2010

Na Elizabeth Mtaja 

Mke wa Raisi Jakaya Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanaake na Maendeleo (WAMA) Mama Salma, amesema teknolojia ya komputya ina mchango mkubwa katika kuleta Maendeleo ya Wanawake nchini .

Alitoa kauli hiyo jana alipopokea msada wa komputya 100 zenye thamani ya dola za Marekani 60,000 zilizotolewa na kampuni ya HUAWEI technology kutoka China, ikiwa ni mwendelezo wa Siku ya Wanawake Duniani iliyoadhimishwa Machi 8 mwaka huu.

Matumizi ya komputya ni njia mojawapo ya kumuimarisha mwanamke katika kujifunza na kujiimarisha katika biashara alisema

“Kwa kuwa WAMA inalenga kuboresha maisa ya Wanawake na watoto hususan walio katika mazingira magumu naamini teknolojia hii itaezesha kuboresha huduma zetu katika kumpatia mwanamke elimu bora , huduma za afya na kumjengea uwzo kiuchumi”, alisema Mama Salma.

Mama Salam alisema vitendea kazi hivyo walivyopokea vitatoa mchango katika kuwajengea uwezo Wanawake katika shughuli za Maendeleo na kuongeza kuwa ni matumaini kampuni ya HUAWEI itawekeza zaidi nchini kupitia nyanja mbalimbali kwa ajili ya kuwanufaisha wananchi wengi zaidi. Awali Mkurugenzi Mkuu wa HUAWEI Tanzania, Yuan Song alisema mchango huo umetolewa kama njia mojawapo ya kuunga mkono juhudi za Wanawake hapa nchini katika kujiletea Maendeleo.

Komputya hizo zitagawiwa katika shule mbalimbali nchini na kipaumbele kitatolewa kwa shule ya wasichana ikiwamo WAMA- NAKAYAMA iinayomilikiwa na WAMA huko Nyamisati wilayani Rufiji.  

Site Search