WAMA yasikitishwa
na mimba , utoro shuleni, Machi 27 2010
Na Tabia Daffo, Babati
Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo
(WAMA), Mama Salma Kikwete amesikitishwa na ukubwa wa tatizo
la mimba na utoro kwa Wanafunzi wa mkoani Manyara.
Hali hiyo ilijitokeza baada ya Mkuu wa Mkoa
wa Manyara Henry Shekifu, kumweleza Mama Salma kuwa tatizo la
mimba na utoro limekuwa likirudisha nyuma Maendeleo ya sekta
ya Elimu.

Mama Salma ambaye jana alitembelea na kuzungumza
na Wanafunzi wa shule za masingi na sekondari Bonga wilayani
hapa alielezwa kuwa kati ya Wanafunzi 1,155 walioachwa shule,
1097 ni watoro na 47 walipata mimba wakiwa shuleni.
Kufuatia hali hiyo Mama Salma aliwataka Wanafunzi
kutumia fursa za Elimu wanazopata ili kutimiza malengo wanayojiwekea.
Pia aliwataka kutambua wajibu mkubwa walionao katika kujipenda
na kujilinda, ili kuhakikisha wanahitimu mafunzo na hatimaye
kulitumikia taifa.
|