..NEWS & EVENTS

Mwenyekiti WAMA azindua Mwongozo wa Makanisa wa Kupambana na Unyanyapaa na Ubaguzi Dhihi ya Watu Wanaoishi na Virusi Vya Ukimwi na Ukimwi, Dar es Salaam- Septemba 05, 2009

Mwenyekiti wa WAMA Mheshimiwa Mama Salma Kikwete amezindua rasmi mwongozo wa makanisa wa kupambana na unyanyapaa na ubaguzi dhihi ya watu wanoishi na virusi vya Ukimwi na Ukimwi uliofanyika katika Hoteli Blue Pearl Dar es Salaam, tarehe 05 Septemba 2009.

Mwongozo huo uliandaliwa na Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) yenye lengo lakuelekeza wajibu wa Wakristo na jamii kwa ujumla katika kuepuka kuwanyayapaa na kuwabagua watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI.

Mheshimiwa Mama Kikwete ambaye alikuwa mgeni rasmi alisisitiza umuhimu wa Watanzania kwenda kupima, wanandoa kuwa waaminifu kwenye ndoa zao na vijana ambao hawajaoa wala kuolewa wasubiri hadi watakapooa au kuolewa.

" Kijana wa kike usikubali kudanganywa na fataki. Jiamini, Jiheshimu na Jilinde. Fanya maamuzi ambayo hayatakuletea kupata virusi vya UKIMWI." alisisitiza Mama Kikwete.

Uzinduzi huo ulihudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo: Mheshimiwa Baba Askofu, Peter Kitula- Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania, Baba Askofu John Nkola, Mwenyekiti wa Kamati ya Sheria na Katiba ya CCT , Ndugu John Mapesa, Katibu Mkuu Jumuiya ya Kikristo Tanzania, Mwakilishi kutoka Bakwata na Ndugu Milicent Obaso, Mwakilishi wa USAID.

Site Search