Mwenyekiti
WAMA awashukia wanaume wanaokwepa kupima afya, Machi 27, 2010
Na Selina Wilson, Babati
Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo
(WAMA), Mama Salma Kikwete amewacharukia wanaume wanaoshindwa
kujitokeza kupima afya zao, hivyo kukwamisha mipango ya maendeleo.
Hilo linatokana na taarifa ya Mkuu wa Mkoa
wa Manyara , Henry Shekifu, kuwa asilimia 85 ya wanaojitokeza
kupima virusi vya ukimwi ni wanawake, huku wanaume wakiwa asilimia
15 tu.
Baadhi yenu mnawakandimiza wanawake kwa kuwa
tu nyinyi ni wanaume, basi onyesheni uanaume kwa kujitokeza
kupima virusi vya ukimwi ilimjue afya zenu na mjipange kuishi
kwa kujitambua, “ alisema”

Alisema kwa kujitokeza kwao kupima afya wanakwamisha
mipango ya maendeleo, kwa kuwa kila mwaka hupangwa bajeti ya
mahitaji ya dawa na vifaa kulingana na idadi ya wahitaji.
Mama Salma alisema kiwango cah maambukizi ya
virusi vya ukimwi cah asilimia 1.6 mkoani Manyara kitakuwa si
sahihi kwa kuwa wanaume wengi hawataki kupima afya zao.
|