..FOUNDATION NEWS

WAMA yawamwagia mamilioni wanawake, Machi 28, 2010

Na Selina Wilson, Manyara

WANAWAKE mkoani Manyara wameendelea kuneemeka kwa kuwezeshwa sh. Milioni saba toka Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA).

Fedha hizo zilitolewa na Mwenyekiti wa WAMA, Mama Salma Kikwete katika ziara yake ya siku mbili mkoani humo, kukagua shughuli mbalimbali zikiwemo za ujasiriamali za wanawake.

Salma alikabidhi hundi ya sh. Millioni tatu kwa Umoja wa Wanawake wa Tanzania (UWT) , mkoa wa Manyara. Kwa upande wa Wilaya ya Mbulu alitoa hundi ya sh. Millioni nne kwa vikundi vinne vya wanawake.

Akiwa wilayani Babati alikagua shughuli za bidhaa zinazotengenezwa na wanachama wa UWT, ambapo mamia ya wanawake walikusanyika katika ukumbi wa CCM wilayay hiyo na kumwonyesha bidhaa mbalimbali.

Akiwa Mbulu Mwenyekiti huyo wa WAMA alizindua utoaji mikopo ya sh. 500,000/= kwa wanawake 95 Fedha hizo zilitolewa na WEDAC.

Akizungumza jitihada za ukombozi kwa wanawake , Salma aliwataka kinamama kutotegemea mapato ya wanaume bali watafute kwao.

“Tusikae kusubiri kinababa mimi nilfundisha mpaka dakika ya mwisho bial kuangalia uwaziri wa mume wangu niliacha baada ya yeye kutangaza kuwania urais “

Aliwataka wanawake kushirikiana kusaka maendeleo na malezi ya familia.

Site Search