Mwenyekiti
wa WAMA Mhe. Mama Salma Kikwete kuhutubia mkutano wa wanawake
wa dunia , Mei 22, 2010
Na Mwandishi Maalum,Beijing
MKE wa Rais Mama Salma Kikwete leo atahutubia
mkutano wa wanawake wa dunia katika kuelezea mafanikio aliyoyapata
katika taasisi yake ya wanawake na maendeleo (WAMA) na juhudi
zake binafsi za kusaidia ugonjwa wa saratani ya shingo ya kizazi.
Mama Kikwete ambae ametajwa kuwa mfano bora
kwa wake wa marais wa Afrika kufuatia taasisi yake ya WAMA kujikita
zaidi katika kusaidia jamii na hasa jitihada zake binafsi za
kusaidia wanawake,afya, na watoto wanaoishio katika mazingira
hatarishi.
Katika mkutano huu wa dunia unafikia kilele
chake leo, katika ukumbi wa Marriot city Hall uliopo katikati
ya jiji la Beijing na karibu wajumbe 1000 wanaohudhulia
mkutano huo wana hamu kubwa ya kusikia mafanikio aliyopata Mama
Kikwete katika kutimiza malengo yake ya WAMA.
Juzi katrika ufunguzi wa mkutano huo, Rais
wa Global Summit of Woman , Bibi Irene Natividad alimtaja
Mama Kikwete kuwa ni mfano bora wa wake wa marais kutoka Afrika
na kusema kuwa jitihada zake binafsi zinaweza kuwa fundisha
kwa wake wengine wa marais kutoka Afrika na wanwake wengine
wanaopenda kusaidia jamii.
.jpg)
Awali jana mchana Mama Kikwete alialikwa katika
mkutano wa kuwatambulisha watu mashuhuri waliohudhulia mkutano
huo, lakini asilimia kubwa ya maswali yalielekezwa kwa Mama
Kikwete baada ya kutakiwa kueleza kwa nini alianzisha taasisi
ya WAMA na madhumuni yake makubwa yalikuwa ni nini.
Akijibu maswali kwa kujiamini , Mama
Kikwete Kiwete alisema madhumuni makubwa ya kuanzishwa kwa WAMA
ni kumuendeleza mwanamke kielimu, kiafya na kusaidia watoto
wanaoishi katika mazingira hatarishi na wale wanaishi katika
mazingira hatarishi.
Alisema kuwa vitu vingi amekuwa akifanya kupitia
taasisi yake ya WAMA kusaidia wanawake wa Kitanzania ikiwemo
suala la elimu kwa kuwa ndiyo njia pekee ambayo inaweza kumkwamua
mwanamke katika maisha ya chini na hili amekuwa ameanza kwa
wasichana wadogo kuwasisitiza umuhimu wa elimu na kujiepusha
na mimba za utotoni na hususan swala la kujiepusha na ugongwa
wa ukimwi.
Pia alisema katika serikali ya awamu ya nne
inayoongwa na mumewe imeweza kupiga hatua kubwa katika suala
la kumtetea mwanamke, kwani wanawake wengi wamekuwa wakipewa
nafasi za uongozi kwa asilimia kubwa na hata masuala mbalimbali
ya kimaendeleo.
Mama Kikwete aliendelea kusema kuwa mbali ya
hiyo serikali imeweza kusaidia kwa kiasi kikubwa kuanzishwa
kwa benki ya maendeleo ya wanawake ambayo itakuwa
hatua muafaka ya kuwawezesha wanawake kiuchumi.
“Ni ushahidi mwingine kwamba serikali yetu
inawajali wanawake wa Tanzania na inayodhaamira ya dhati ya
kuinua hali zao za kimaisha na kuwepo kwa benki hiyo kumetoa
fursa kwa wanawake wa Tanzania kutumia huduma zake za kujiletea
maendeleo na kuondokana na umaskini.
Awali mchana jana alikutana na viongozi wa
chama cha wafanyabishara wanawake wa China na wale wa Tanzania
katika kubadilishana mawazo na kuona uwezekano wa kusiadia katika
masuala mbalimbali ya kibiashara katika ya nchi hizi mbili.
|