..NEWS & EVENTS

Wananchi wilayani Bagamoyo watakiwa kuacha tabia ya kuchoma moto Shule
Na Anna Nkinda – Maelezo, Bagamoyo- 5/10/2009

Wananchi wilayani Bagamoyo wametakiwa kuachana na tabia ya kuchoma moto shule kitendo ambacho kinachangia kwa kiasi kikubwa kurudisha nyuma maendeleo ya elimu wilayani humo.

Wito huo umetolea jana na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete wakati akiongea na wananchi wa wilaya hiyo kwa nyakati tofauti katika vituo vya afya Kiwangwa, Miono, Lugoba na shule ya sekondari ya wasichana Mandera.

Mama Kikwete alisema kuwa wilaya hiyo imekuwa na matukio mengi ya uchomaji wa moto katika mabweni na shule ambazo zimejengwa kwa gharama kubwa na wananchi kwa kushirikiana na serikali.


“Mkoa huu uko nyuma sana katika maendeleo ya elimu sasa kama mtaendelea kuzichoma moto shule sijui kama kutakuwa na maendeleo ili kukabiliana na taizo hili nawaomba muwe makini kuzilinda shule zenu na kama itatokea mtamfahamu mtu anayezichoma atajwe”

“Wanaozichoma shule hizi mnawafahamu hivyo basi ni vyema kila mtu akawa mlinzi kwa mwenzake kitendo ambacho kitasaidia kutokutokea tena kwa tatizo kama hili”, alisema Mwenyekiti huyo wa WAMA.

Akisoma taarifa ya shule ya Sekondari ya wasichana Mandera Mwalimu mkuu Rose Umila alisema kuwa serikali kwa kuona umuhimu wa elimu kwa mtoto wa kike iliamua kuiteua shule hiyo kuwa shule ya kipekee ya serikali ya wasichana katika wilaya hiyo mwanzoni mwa mwaka huu hadi sasa inajumla ya wanafunzi 278 .

Mwalimu Umila alisema, “Shule hii inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na upungufu wa mabweni, thamani, hakuna maabara na maktaba pamoja na upungufu wa majengo ya madarasa.Pia kuwepo kwa watoto wengi wanaotoka katika mazingira magumu na hivyo kushindwa kulia michango ya shule”.

Aliendelea kusema kuwa hiyo ambayo itazinduliwa rasmi mwaka 2010 inampango wa kujenga vyumba vitano vya madarasa kwa ajili ya kuwapokea wanafunzi wa kidato cha kwanza hapo mwakani.

Mama Kikwete alitoa zawadi ya jezi jozi moja pamoja na mipira miwili kwa wanafunzi wa shule hiyo ambayo wataitumia katika kucheza mpira mara baada ya kumaliza shughuli za masomo ili kujiimarisha kimwili.

Taasisi ya WAMA pia ilitoa vitu mbalimbali katika zahanati ya Kiwangwa yakiwemo magodoro matano, Derivary Kit moja, kitanda cha Hospitali kimoja, mashuka 20, kitanda maalum cha kujifungulia kimoja, Saction pump moja na katika vituo vya Afya Miono ilitoa mashuka 20, Derivary Kit moja, itanda vya hospitali vine,sanction pump moja, hot air sterilirez moja, syringe needle mabox mawili, magodoro 10.

Katika kituo cha afya Lugoba taasisai hiyo ilitoa vitanda maalum vya kujifungulia vinne, sanction machine (ya umeme) moja, vitanda vya hospitali viwili, derivary Kit moja, Oxygen concentrator moja, vacuum extraction moja, sunction pump moja, mashuka 20, magodoro mawili, Adult scale moja, Infants scale moja, Theater boot moja na katika hospitali ya wilaya ya Bagamoyo ilitoa mashine moja ya kufulia.

Site Search