Wazazi na Walezi waaswa kuhimiza watoto kusoma Quran ili kujenga kizazi kilicho bora na kuongeza ubunifu katika elimu dunia - 05 Septemba, 2009
Mwenyekiti wa WAMA Mheshimiwa Mama Salma Kikwete amewaasa wazazi, walezi na wanafamilia kuhimiza watoto wao kusoma Quran na kufuata maadili ya kiislam ili kujenga kizazi kilicho bora na kuongeza ubunifu katika masomo ya elimu.
"Elimu ni amri ya kwanza aliyopewa mwanadamu kwa kuambiwa Iqraa yaani soma! Hivyo ni wajibu wetu sisi wazazi na walezi kuhakikisha watoto wetu wanasoma Quran ambayo pia humjengea mtoto uwezo kiakili na kumsaidia katika masomo ya elimu dunia." Alisema Mama Kikwete.
Mama Kikwete alitoa nasaha hizo kwenye mashindano ya Quarani Tukufu iliyoandaliwa na jumuiya ya Wanamwake wa Kiislam Tanzania yaliyofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es salaam tarehe 05 Septemba, 2009.
Kwenye mashindano hayo waalimu walioandaa wanafunzi walioshinda walipata laki moja (100,000/=) na wasomaji kumi bora walipata laki moja (100,000/=) kila mmoja. Pia wanafunzi pamoja na mayatima walifuturishawa siku hiyo.
|