..NEWS & EVENTS

WAMA yachangia 1.5 ml. Kusaidia Timu ya Viziwi ya Mkoa wa Pwani kushiriki Michezo ya Kimataifa– Tumbi, Kibaha- Agosti 27, 2009

Mwenyekiti wa WAMA Mheshimiwa Mama Salma Kikwete amechangia shilingi millioni moja na laki tano kwa ajili ya kusaidia Timu ya Viziwi ya Pwani kushiriki kwenye michezo ya kimataifa wakati wa warsha ya ufunguzi wa Mkakati wa Kuendesha Michezo ya viziwi iliyofanyika wilayani Kibaha.

Akisoma risala kwa Mgeni rasmi Mwenyekiti Mstaafu wa Chama na Mweka hazina Klabu ya Michezo ya Viziwi Bw. Daudi Kulangwa amesema kuwa viziwi wanapenda sana michezo na wanaleta maombi kwa Mgeni rasmi ili wapatiwe viwanja vya michezo, vifaa, vitendea kazi vya ofisini na ushiriki wa michezo ya kimataifa. Walimweleza Mama Kikwete kuwa wanadaiwa shillingi millioni tatu. (3,000,000/=) kwa ajili ya ada ya usajili wa kimataifa ya shirikisho la viziwi duniani.

Mama Kikwete ambaye alikuwa Mgeni Rasmi kwenye warsha hiyo alisema amezielewa changamoto wanazokabiliana nazo na akahaidi kusaidiana nao pamoja na kuwapa nusu ya hela wanayodaiwa na akawomba na wadau wengi washirikiane kwa pamoja kutatua matatizo hayo.

Mama Kikwete pia aliikaribisha Timu ya viziwi kutermbelea mradi wa WAMA- wa Umoja wa Wakulima Hoyoyo, Mkuranga unaofanya kazi za Kilimo cha Paprika na Ufugaji wa Kuku wa Kienyeji na Mbuzi ulioko chini ya Kitengo cha Uwezeshwaji wa Wanawake.

Alieleza pia taasisi yake imekuwa ikiwasaidia watu wanoishi katika mazingira magumu kwa kupitia vitengo vyake vinne: Elimu, Afya, Uwezeshwaji wa Wanawake na Watoto Yatima na Wanaoishi Katika Mazingira Magumu.

Site Search


More News
Tani 372.4 za chakula Bagamoyo kukabiliana na Njaa
Wanawake Morogoro watakiwa kuwa mstari wa mbele ktk shughuli za maendeleo
Serikali imetumia Ml 105 kujenga shule ya sekondari ya Kilakala
Wanafunzi 287 wapata ujauzito Kwa kipindi cha miezi Tisa
Wanaume watakiwa kushiriki katika kupunguza vifo vya mama wajawazito
Wananchi Bagamoyo watakiwa kuacha tabia ya kuchoma Shule
  Wazazi waaswa kuhimiza watoto kusoma Quran ili kujenga kizazi kilicho bora na kuongeza ubunifu katika elimu dunia
Mwenyekiti WAMA azindua Mwongozo wa Makanisa wa Kupambana na Unyanyapaa na Ubaguzi Dhihi ya Watu Wanaoishi na Virusi Vya Ukimwi
WAMA yachangia 1.5 ml. Kusaidia Timu ya Viziwi ya Mkoa wa Pwani kushiriki Michezo ya Kimataifa
Mwenyekiti WAMA aomba mashirika na watu binafsi kusaidia wanaoishi ktk mazingira magumu
Management Science for Health (MSH) facilitates WAMA Monitoring and Evaluation System Training
WAMA the 2nd in NGO Sector in Nane Nane Exhibition in Dodoma
WAMA and USAID Confirm Partnership for Adolescent Early Pregnancy Prevention
Hon. Jackie Winters (State Senator – Oregon ) and Dr. James Luce visit WAMA to Discuss Collaboration
Wanawake 80,000 wanaweza kupoteza maisha na milioni mbili na nusu kupata ulemavu ikiwa juhudi za dhati hazitafanyika
Mama Salma Kikwete Asisitiza Kuundwa Kwa Sekretariati ya Kudumu ya OAFLA
Hon. Salma Kikwete insist men to undergo HIV/AIDS testing- June 27, 2009 in Bagamoyo
Magindu Secondary School got assistance from WAMA Foundation
Hon. Salma Kikwete asks for more people to contribute on ending Child Hunger
Mama Kikwete donates Tz. 2 million to support Choir of St. Kizito of Makuburi Catholic Church
First Lady encourages Islamic Girls to join Science Subjects – Hijab Day Celebration
Mama Kikwete calls for African First Ladies sustainable partnership in Los Angeles California